About

Friday, May 25, 2012

IMANI ZA KISHIRIKINA KWENYE STAGE KENYA ZAMPATA NYOTA NDOGO.


Kumbe sio bongo tu ambako imani za kishirikina ni moja kati ya stori kubwa kwa baadhi ya wasanii kwa siku za karibuni, stori kutoka 254 Kenya taifa la Ocampo 6 ni kwamba wasanii Ally B na Nyota dogo walishindwa kuperform kwenye show huko Mombasa kitu ambacho kinaaminika kuwa ni kutokana na imani za kishirikina kwa sababu wasanii wengine wa Mombasa wakiona wenzao wanafanikiwa huwa hawapendi, ndio wanaanza kulogana.
Ally B ambae ni msanii maarufu Kenya kwa sasa akiwa tayari kapiga kolabo na wakali kama Size 8 na Prezzo, amethibitisha kwa kusema “huwa nakwenda kwenye show na CD nne au tatu lakini wakati wa Show time CD zangu zote ziligoma kucheza, alipokuja Nyota Ndogo pia CD zake zote zikakataa kucheza basi ikabidi tuwaombe mashabiki tuimbe akapela kwa sababu hata Laptop ilipoletwa baadae kuokoa jahazi nayo ilikataa kusoma CD, wapo mashabiki walioelewa na wengine hawakuelewa”

Facebook comments brought to you by bongo6