About

Thursday, March 8, 2012

OSHA YAENDELEA KUVIFUNGIA VIWANDA AMBAVYO HAVIZINGATII USALAMA NA AFYA MAHALI PA KAZI


Mfanyakazi wa Kiwanda cha Kamal Steel akiwa anafanyakazi kwenye eneo hatari la kutengeneza nondo,huku akiwa hana viatu maalumu vya kuweza kumkinga asiweze kudhurika endapo ajali itatokea.
 
Mfanyakazi akiwa anafanya kazi katika eneo hatarishi huku akiwa hana Maski wala "gloves" badala yake akiwa amefunga kitambaa kumzuia na gesi hatarishi zinazoweza kumpata kutokana na vyuma hivyo.
 

Mkurugenzi wa Usalama na Afya toka (OSHA) ndugu Alex Ngata akiongea na waandishi wa Habari kwenye Kiwandani Kiwanda cha Kamal steel kuwaeleza maeneo ya kiwanda hicho yaliyofungiwa.

 
Meneja wa Kanda ya Pwani wa OSHA ndugu Benjamini Kisungwe akiwaeleza waandishi wa habari mojawapo ya eneo ambalo ni hatari likiwa wazi bila ya tahadhari yoyote inayotolewa kwa wafanyakazi na watu wanaopita eneo hilo.

Wakala wa Afya na Usalama Mahali Pa Kazi (OSHA) imeendelea na zoezi lake maalum la kukagua viwanda vinavyotengeneza Nondo jijini Dar es Salaam,. Kiwanda cha Kutengeneza Nondo cha Kamal Steel ni mojawapo ya Viwanda ambavyo rungu la kuvifungia limekikumba.

 Mkurugenzi wa Usalama na Afya toka OSHA ndugu Alex Ngata amekifungia Kiwanda cha kutengeneza chuma cha Kamal Steel, kwa kukiuka Usalama na Afya kwa wafanyakazi wa kiwanda hicho.

Katika Ukaguzi wa kushitukiza uliofanywa na Wakala wa Afya na Usalama Mahali Pa kazi (OSHA), umekuta hali isiyoridhisha kwa wafanyakazi wa kiwanda hicho, wakiwa wanafanya kazi katika mazingira hatarishi.

Kabla ya kukifungia Kiwanda hicho, OSHA ilitoa Notisi ya wiki mbili ili wamiliki wakiwanda hicho wahakikishe wanazingatia Sheria ya Usalama na Afya Mahali Pa kazi, hata hivyo baada ya kufanya ukaguzi wa kushitukiza wamekuta hakuna maboresho yoyote yaliyofanyika, na hivyo kuamua kufunga baadhi ya maeneo ambayo yalionekana kuwa yanahatarisha zaidi usalama kwa wafanyakazi, baadhi ya maeneo yaliyofungiwa ni pamoja na sehemu ya kuyeyushia chuma, na eneo la kukusanyia vyuma chakavu.

Facebook comments brought to you by bongo6