Wananchi wa kijiji cha Mirongoine pamoja na wale wa kijiji cha Moshono Jijini Arusha leo wameandamana hadi Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha,Mh. Magessa Mulongo kupinga kuamishwa katika makazi yao pamoja na kuomba kuachiwa huru kwa maeneo yao ambayo wamedai kuwa yanamilikiwa na wanajeshi ili waweze kufanya maendeleo.
Kiongozi wa Wananchi hao walioandamana leo hadi kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha,aliyejulikana kwa jina la Emmanuel Masamaki akitoa malalamiko yao mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha,Mh. Magessa Mulongo (hayupo pichani) leo Jijini Arusha.Picha na Woinde Shizza.