![]() | |
Akiwa nyumbani kwake na Mwalimu ambae ni sawa na mjukuu wake |
![]() |
Nyumba anayoishi. |
![]() |
Akiwa darasani na wanafunzi wenzake. |
![]() |
Akiwa darasani na wanafunzi wenzake. |
Mafanikio ya mwanga aliouona hayajatajwa na yeye peke yake, hata walimu wake wamethibitisha mabadiliko kwake wakisema mwanzoni alikua nashikiwa kalamu lakini sasa anashika mwenyewe.
Yani mpaka sasa bibi priscila anauwezo wa kuongoza darasa ambalo wanafunzi wengine waliobaki ni kama vitukuu vyake, tayari anaweza kusoma baadhi ya maneno ya kiingereza kama Apple, Lion, Mango n.k
NTV KENYA wamesema Bibi huyu mwenye umri wa miaka 90, anasema ni ukweli kwamba ana enjoy kuwepo darasani kila wakati manake hata hao wanafunzi wenzake ambao ni sawa na vitukuu vyake wanampenda na wanampa ushirikiano, wanamuazima vitu kama vile kalamu na anapokosa kwenda shule huwa watoto wanakosa furaha.
Priscillah amesema hajui ataishia wapi kwenye swala la kusoma ila anachomuomba Mungu ni kulinda macho yake ili asishindwe kusoma vitabu.
Msikilize Bibi mwenyewe akiongea hapo chini…..